32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mgodi wa Buzwagi watenga bilioni 1.3/- kupanda miti

Mgodi wa wazi wa Buzwagi
Mgodi wa wazi wa Buzwagi

Na HARRIETH MANDARI,

KATIKA jitihada za kutunza mazingira, mgodi wa dhahabu wa Buzwagi umetenga shilingi bilioni  1.3/-(Dola za Kimarekani laki sita)  kupanda miti milioni 1.6 katika eneo linalolizunguka.

Mradi huo wa uoteshaji miti, ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya mazingira kwa sekta ya madini nchini.

Akizungumza na Mtanzania wakati wa ziara ya waandishi katika mgodi huo, Meneja uendelevu wa mgodi huo, George Mukanza alisema moja ya mipango ya ya mgodi huo ambao ni mali ya kampuni tanzu ya ACACIA ni kuhakikisha eneo lote la machimbo linakuwa na miti ya kutosha na uoto wa asili.

Mgodi wa Buzwagi  ambao ulianza uchimbaji mwaka 2009, unategema kuendesha shughuli zake kwa miaka 15. Mgodi huu unaochimbwa kwa mfumo wa machimbo ya wazi  na unakadiriwa kuwa na kiasi cha ujazo wa dhahabu ardhini kipatacho ounces 0.625***.

Kwa wastani uzalishaji wa dhahabu mgodini hapo  ni kiasi cha wastani wa gramu 1.32 ambazo hupatikana kwa tani moja ya mawe yaliyochimbwa.

“Ni matarajio yetu kuwa itakapofika wakati wa kufunga mgodi huu tutahakikisha kuna miti ya kutosha katika maeneno haya ili kuwa na uoto wa asili. Kwa upande wa mashimo yapo matumizi mengi tu yatakayofaa ikiwemo chuo cha madini, mabwawa ya samamki au hata bwawa la kuhifadhi maji ambalo litanufaisha jamii inayouzunguka mgodi,”alisema.

Mukanza aliongeza kuwa,  suala la uhifadhi mazingira mgodini hapo ni moja ya agenda zilizopewa kipaumbele na ambalo liko kisheria ambapo katika miaka miwili iliyopita zaidi ya tani 1000 za kemikali taka za madini zimeharibiwa   kwa mfumo wa  kuzingatia uhifadhi mazingira.

Meneja uzalishaji  wa mgodi huo, Rodney Burgess  alisema mgodi wa Buzwagi hauna athari kubwa kwa mazingira kwani ardhi yake ina kiasi kidogo sana cha miamba ya acid na kwamba matumizi ya kemikali ya aina ya  ‘Cyanide’ ambayo baada ya matumizi ya uchenjuaji dhahabu huchakachuliwa ili kuondoa madhara ardhini ndiyo inatumika.

“Katika kipindi cha mwaka huu wa fedha, mgodi wa Buzwagi umetumia kiasi cha Dola za kimarekani 1.4milioni  kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendelelo zikiwemo ujenzi wa shule za sekondari na za msingi, uchimbaji visima, michezo, ujenzi wa vituo vya afya, na ujenzi wa barabara,” alisema.

Kwa upande wa ujenzi wa barabara, katika mwaka huu wa fedha jumla ya kilomita 12 za barabara zimejengwa katika vijiji mbalimbali kuzunguka mgodi huo ambao unategemewa kufungwa mwezi machi mwaka 2018 kama kutakuwa hakuna ugunduzi mwingine wa madini katika  eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles