24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mgodi wa Buckreef watenga Milioni 321 kusaidia jamii

Anna  Ruhasha, Geita 

Kampuni ya Mgodi wa Buckreef imetenga Sh milioni 321 kwa ajili ya maendeleo ya jamii hususan nyanja ya elimu, afya na maji lengo likiwa ni kupunguza changamoto  zinazowakabili wakazi wa Halmshauri ya Wilaya ya Geita vijijini mkoani humo.

Mbunge  wa Geita  Mjini,  Constanine Kanyasu akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Rasilimali Watu wa Kampuni  ya Mgodi wa  Buckreef, Amerid Msuya. Picha na Anna  Ruhasha.

Akizungumza leo Septemba 18, mbele ya mbunge wa Geita mjini, Costantine Kanyasu alipotembelea banda hilo, Meneja Rasilimali watu wa Mgodi wa Buckreef, Amerida Msuya, amesema wamejikita kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuboresha huduma muhimu.


Msuya amesema kuwa mgodi wa Buckreef ambao unamilikiwa kwa ubia kati ya  Tanzania kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inayomiliki asilimia 45 na mbia ambaye ni Tanzamu 200, inayomiliki asilimia 55, amesema wametenga Dola milioni 74 kwa ajili ya ujenzi wa mgodi wa kisasa.

“Lakini wakati tunaendelea na ujenzi wa mgodi tayari tunatoa huduma kwa jamii  mfano mpaka sasa tumejenga vyumba vya madarasa katika shule  ya msingi Tembo  na tumekabidhi madawati katika shule ya Sekondari ya Kasem,” amesema Msuya.

Upande wake, Mbunge Kanyasu amesema kilio cha wananchi na serikali ni kuona  uwekezaji huo unajitoa zaidi katika kutekeleza shughuli za kijamii kama sheria  inavyoelekeza ambapo pia amepongeza kuona tayari wameanza toa mchango  kwenye jamii inayowazunguka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles