Mghwira aagiza Mkurugenzi Mwanga asilipwe mshahara kwa kushindwa kujibu swali

0
1051

Upendo Mosha, Moshi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Zefrin Lubuva asilipwe mshahara wa Februari hadi atakapojirekebisha.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mghwira kukasirishwa na kitendo cha mkurugenzi huyo kushindwa kujibu maswali aliyomuuliza kwanini halmashauri hiyo imeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.

Sakata hilo limetokea leo Ijumaa Februari 14, katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya mkoa cha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika leo.

“Mkurugenzi wa Mwanga kila wakati umekuwa ukishindwa kujibu maswali vile inavyopaswa sijajua ni nani anakulipa mshahara, ila mamlaka inayohusika kukulipa isikulipe mshara wa mwezi huu,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here