31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Mgambo ahukumiwa kwenda jela miaka miwili

Na UPENDO MOSHA-SAME

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro, imemhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka miwili, askari wa Jeshi la Akiba (mgambo), Tumaini Mgonja.

Mtuhumiwa huyo, alihukumiwa kwenda jela jana baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh milioni 2.5 huku akikiri makosa matano kati ya mashtaka 13 ya kuomba na kupokea rushwa yaliyokuwa yakimkabili.

Katika shtaka hilo, Mgonja na mwenzake, Dausoni David, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bwambo, wilayani Same, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same, wakikabiliwa na mashtaka 13 ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh laki sita.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo, Judithi Kamala, alidai kuwa aliamua kutoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ambao haukuacha shaka yoyote.

“Mshtakiwa nakuhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni 2.5 kwani kosa hilo ulilitenda kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/17,” alisema Hakimu Kamala.

Kwa upande wa mshatakiwa wa pili ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, alikana mashtaka yanayomkabili na mahakama hiyo itaanza kusikiliza shauri lake, Aprili 18, mwaka huu.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoa wa Kilimanjaro, Suzan Kimaro, aliieleza mahakama hiyo kwamba wazazi 10 waliwatuhumu watuhumiwa hao, kwamba wanawadai rushwa kwa kosa la kuchelewa kuwapeleka watoto wao kujiunga na masomo ya sekondari mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles