Mohamed Hamad, Kiteto
Watu 154 ambao kati yao 13 ni wanawake, wamehitimu mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) Kijiji cha Ndaleta wilayaniKiteto mkoani Manyara na kutakiwa kukabiliana na vitendo vya uhalifu uliokithiri.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa, akizungumza na wahitimu hao leo Jumanne Desemba 18, amewataka kutambua kuwa serikali inatambua uwepo wao na kuwataka waanze kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
“Ndaleta ni eneo lililokithiri kwa vitendo vya kihalifu, ninyi jeshi la akiba mtakuwa msaada mkubwa kwetu kukabiliana uhalifu huu,” amesema Magesa.
Akizungumzia ajira mkuu huyo wa wilaya amewataka wahitimu hao kutambua kuwa fursa ziko nyingi na kuwataka kuwa na nidhamu na kuepuka vitendo viovu.
Akisoma risala ya wahitimu, Jamali Kiondo, kwa niaba ya wahitimu wenzake walimwomba mkuu huyo wa wilaya kuwapa kipaumbele katika ajira.