29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mfundishe mtoto usafi wa mwili

mtoto

USAFI ni tabia ambayo  mtoto anapaswa kufundishwa  pindi tu anapoanza kujitambua.

Kumfundisha mtoto usafi unapaswa kuzingatia katika nyanja zote yaani kumuelekeza kuhusu usafi wa mwili pamoja na mazingira yanayomzuguka.

Baadhi ya vijana wengi ambao wana tabia za uchafu ukifuatilia cimbuko lao unakuta kuwa chanzo cha hali hiyo ni kutopata muongozo mzuri kutoka kwa wazazi wa jinsi ya kujisafisha na kufanya usafi  wanapokuwa watoto.

Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya mzazi ni kumfundisha mtoto usafi binafsi yaani kumuelekeza jinsi ya kujisafisha mwili wake na kujitunza.

Hatua za kwanza za awali za kumfundisha usafi mtoto ni pamoja kumfundisha  utaratibu kujisafisha mikono mara kwa mara ili kuepuka kula vyakula akiwa na mikono michafu.

Mfundishe mtoto jinsi ya kuosha mikono pindi  anapotoka chooni ama anapokuwa katoka  kucheza  ili kuondoa bakteria huenda alipokuwa huko alishika vitu kushika uchafu wa aina yeyote ili asije akajisahau anapotaka kula.

Mbali na mikono pia unapaswa kumfundisha jinsi ya  kusafisha  macho,mdomo  na pua,viungo hivi vyote haviitaji kuonekana vikiwa vichafu,usafi wa mdomo unaenda sambamba na kusafisha meno.

Mtoto lazima afundishwe kusafisha  mdomo kwa maana ya kupiga mswaki  na kusafisha meno yake kwa ufasaha ili kusweza kuondoa hatari ya kuoza meno.

Hakikisha mtoto hashiki macho akiwa na mikono michafu ama akiwa ameshagusa kitu chochote kinachoweza kudhuru kama pilipili ama dawa yeyote.

Jambo lingine la msingi unalopaswa kumfundisha mtoto  ni kuwa na mazoea ya kuoga hasa  nyakati za usiku.

Wazazi wengi wamegundua kwamba  mtoto akioga usiku ndiyo njia yake pekee ya kuwa na amani kabla hajaenda kulala.

Kuoga usiku pia kunaweza kukamsaidia mtoto kuamka mapema pia kunamfanya mtoto anakuwa na nguvu ya kuanza siku inayofuata bila kuwa na vikwazo vya uvivu.

Katika vitu hivyo muhimu endapo utaamua kumuacha mtoto ajiongoze mwenyewe na mtoto hakawa hana hulka ya usafi unaweza ukachangia kuzalisha  kijana  mchafu hali itayochangia apate shida katika jamii itakayomzunguka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles