30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei washuka kutoka asilimi 4.2 hadi 4.0

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi Januari, mwaka huu umepungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Februari 8,2022 jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu fahirisi za bei za Taifa kwa mwezi Januari mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii, Ruth Minja akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne, Februari 8,2022.

Amesema kupungua huko kunamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021.

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia Desemba 2021

“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Januari mwaka huu umepungua hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 3.9 ilivyokuwa kwq mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021 na mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula visivyochakatwa,nishati na bili za maji(core inflation)kwa mwezi Januari mwaka huu umepungua pia hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 4.6 ilivyokuwa mwezi Desemba,2021,”amesema Minja.

Ametaja baadhi ya bidhaa zingine zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021 ni pamoja na mavazi kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 2.8.

“Viatu kutoka asilimia 4.6 hadi asilimia 4.4,kodi ya pango kutoka asilimia 4.4 hadi asilimia 1.5,cherehani kutoka asilimia 9.1 hadi asilimia 5.0,simu janja kutoka asilimia 3.5 hadi 3.3.

“Vyombo vya nyumbani kama sahani kutoka asilimia 16.7 hadi asilimia 3.6,luninga kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 1.2 na malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kutoka asilimia 6.6 hadi asilimia 2.9,”amesema

Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu kwa Nchi ya Uganda amesema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu umepungua hadi asilimia 2.7 kutoka asilimia 2.9 kwa mwaka ulioishia Desemba mwaka 2021.

Amesema kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu umepungua hadi asilimia 5.39 kutoka asilimia 5.73 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles