29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei wapungua kwa asilimia 3.2

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi ulioishia Mei, mwaka huu  umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa Aprili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja, alisema kuwa mfumuko wa beiumepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 ya Aprili mwaka huu.

Alisema hali hiyo ina maanisha kuwa kiasi cha mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Mei mwaka 2020,  umepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa Aprili mwaka 2020.

Minja alisema kuwa kushuka kwa mfumo wa bei kumechangiwa na kupungua kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Mei, mwaka huu ikilinganishwa na Mei, 2019.

Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa Mei, 2020 zikilinganishwa na Mei 2019 ni pamoja na matunda kwa asilimia 5.8,viazi mviringo 5.5, mihogo 13.9, viazi vitamu 8.8 na ndizi za kupika 3.0.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa Mei, 2020 zikilinganishwa na bei za Mei, 2019 ni pamoja na mafuta ya taa 14.3, petroli 10.0 na dizeli 12.9.

“Mfumo wa bei kwa baadhi ya vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020 umepungua hadi asilimia 4.4 kutoka asilimia 4.6 kwa mwaka ulioishia Aprili, mwaka huu,” alisema Minja

Alisema hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa Mei, 2020,  Kenya asilimia 5.47 kutoka 5.62, Uganda napo umepungua hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.2 Aprili mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles