27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei wa taifa wabaki asilimia 3.2

RAMADHAN HASSAN -DODOMA

MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020.

Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020.

Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019.

Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3.

Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.

Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.

Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles