30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumo wa Mshitiri utakuwa mwarobaini wa uhaba wa dawa-Serikali

Na Amina Omary, Tanga

Serikali imesema kuwa iwapo Mfumo wa mshitiri (prime Vendor system) ukisimamiwa vizuri utaweza kumaliza changamoto ya uhaba wa dawa na uwepo wa uhakika wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya nchini.

Hayo yameelezwa leo Machi 22, 2023 na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, George Mmbaga wakati akifungua mafunzo ya wawezeshaji wa mfumo wa mshitiri kwa wataalamu wa maabara, famasia na TEHAMA walioko katika ngazi za Halmashauri mkoani hapa.

Amesema kuwa mfumo huo utawezesha upatikanaji wa bidhaa za afya ambazo zinakosekana Bohari ya Dawa (MSD) na hivyo kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

“Mafunzo haya ya lengo la kupata wawezeshaji wa mkoa na Halimashauri wa kutumia mfumo lengo ikiwa ni katika vituo vya kutolea kuwepo na upatikanaji wa dawa na vipimo vya kitabibu Ili kuakisi huduma bora kwa wananchi,”alisema Mmbaga.

Aidha, amewataka Wakurungezi wa Halimashauri kusimamia makusanyo ya Mapato kwenye vituo vya afya Kwa ajili ya kupata fedha za kutosha Kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya sambamba na kusimamia mnyororo wa ugavi wa bidhaa hizo.

Hata hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga, Rehema Maggid amesema Serikali imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali Ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unakuwa kwa asilimia 100.

Amesema ni imani yake kupitia mafunzo hayo washiriki wataweza kuyafanyiakazi na hivyo kumaliza changamoto ya uhaba wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

“Kwa kutekeleza miongozi ya mfumo wa mshitiri tunakwenda kutoa huduma ambao imekusudiwa na wananchi bila ya kuwepo kwa manunguniko ya uhaba wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyetu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles