24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Mfumo wa Android kuondolewa katika Smartphone

BEIJING, CHINA

BAADA ya miezi kadhaa ya mzozo na Marekani kampuni ya bidhaa za kielektoniki  ya Huawei ya nchini China imetangaza kuja na mfumo mpya na kuachana na ule wa Android kwa ajili ya kuboresha simu za mkononi za Samartphones, vipakatalishi na vifaa vingine vya nyumbani.

Mfumo huo ni HarmonyOS  na kampuni hiyo imeutaja kuwa ni bora kuliko wa Android.

Mfumo huo wa Huawei -HarmonyOS unalenga kupunguza utegemezi wake kwa kampuni za Marekani.

Taarifa hii ya Huawei imekuja miezi kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuweka masharti ya kibiashara nchini Marekani yanayoilenga kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine washirika .

Serikali ya Marekani inaishutumu Huawei kwa kuiba siri za kibiashara, na inasema inaleta hatari kwa usalama wa taifa hilo.

Huawei inapinga shutuma hizo na imeamua kuchukua hatua za kisheria kukabiliana na shutuma za Marekani.

Baada ya shutuma hizo , Google, Intel,na makumpuni mengine yanayochangia katika kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na utatuzi wa matatizo ya smartphone walisitisha biashara na Huawei, huku wakihoji juu ya hali ya baaadae ya kampuni hiyo.

Katika kile ambacho Huawei inaonekana kujinasua kutoka katika hali hiyo, Mkurugenzi mkuu wa wa kitengo cha walaji cha Huawei Richard Yu, akizungumza  katika mkutano wa ubunifu alisema mfumo wa HarmonyOS utakuwa tayari kuwekwa katika skrini za kiditali kwenye bidhaa kama vile Televisheni, saa za smart , na magari baadae mwaka huu.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Huawei, kampuni ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani ya mauzo ya smartphone, itaangalia jinsi ya kuuweka mfumo wa HarmonyOS kwenye vifaa zaidi zikiwemo simu zake za mkononi aina ya smartphones.

Muasisi wa Huawei , Ren Zhengfei amesema HarmonyOS inaweza kuwekwa katika hali ya kuwa na maingiliano na kifaa kingine chochote kile.

Kampuni ya Huawei inasema kuwa imeazimia kuendelea kutumia Android , lakini mfumo wa HarmonyOS utatumika kama mbadala iwapo  mambo yataenda haraka .

“Tutaupa kipaumbele mfumo wa Android kwa smartphones, lakini kama hatutatumia Android, tutaweza kuweka mfumo wa HarmonyOS haraka,” Yu alisisitiza.

Alisema kwa kuanzia China itafaidika na mfumo huo wakati kampuni hiyo ikiendelea na mipango ya kuufikisha katika mataifa mengine baadae.

Vita vinavyoendelea vya kibiashara baina ya Marekani na China tayari vimeiathiri Huawei.

Utendaji wa kampuni umeripotiwa kuwa ni dhaifu kufikia hadi mwezi Juni.

Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Counterpoint, karibu nusu ya simu za martphones za Huawei huuzwa nje ya  China.

Yu anasema Huawei ilikuwa imejipanga kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa bidhaa nje ya nchi duniani, jambo ambalo ingelifanikisha kama ingekuwa si vita vya kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles