23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumo Azam wachanganya wachezaji

azam-fcNa THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya Azam FC, Mhispania Zeben Hernandez, amesema tatizo kubwa linalowasumbua wachezaji wake katika mechi za Ligi Kuu Bara ni kushindwa kuuelewa mfumo anaowafundisha.

Juzi Azam FC walikubali kipigo cha kwanza msimu huu baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Simba, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi, Hernandez ambaye ameanza kuifundisha Azam FC msimu huu, alisema kikosi chake kilikutana na timu kubwa yenye wachezaji wazoefu, lakini kosa dogo limesababisha wafungwe na kupoteza pointi tatu muhimu.

“Licha ya kufungwa, wachezaji walionyesha kiwango kizuri, lakini tatizo linalowasumbua zaidi ni kushindwa kuuelewa mfumo ninaowafundisha,” alisema Hernandez.

Alisema mfumo anaotumia kufundisha ni changamoto kwa nyota wake, lakini ataendelea kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili yasijirudie katika mechi nyingine zinazowakabili kwenye ligi hiyo.

Tatizo la Azam FC huenda linasababishwa na mtindo wa klabu hiyo kubadilisha makocha mara kwa mara, kwani baada ya msimu uliopita kumalizika, benchi la ufundi lilifanyiwa mabadiliko.

Kwa upande wake, kiungo wa timu hiyo, Himid Mao, alisema walicheza kwa kujituma uwanjani ili kuhakikisha ushindi unapatikana lakini matokeo yakawa tofauti na matarajio yao.

“Tumecheza vizuri sana lakini sielewi tatizo lilikuwa wapi, kwa sasa tunaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata ili tuweze kupata matokeo mazuri,” alisema Mao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles