28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Mfanyakazi wa mwanamke bilionea Afrika akutwa amekufa

Lisbon, Ureno

MFANYAKAZI wa benki aliyekuwa akisimamia akaunti za kampuni ya mafuta Sonangol, ambayo mwenyekiti wake alikuwa Isabel Dos Santos katika benki ya EuroBic nchini Ureno, amekutwa amekufa mjini Lisbon

Mfanyakazi huyo, Nuno Ribeiro da Cunha mwenye umri wa miaka 45 anahusishwa na kesi ya ufujaji na ulanguzi wa fedha za Isabel ambaye ni mwanamke tajiri barani Afrika, Isabel dos Santos.

Akaunti alizokuwa akizisimamia zilikuwa katika benki ya EuroBic nchini Ureno ambayo Isabel ana hisa.

Kifo chake hicho kilichotokea Jumatano kiliripotiwa Alhamisi muda mfupi tu baada ya waendesha mashtaka nchini Angola kuwataja wote wawili kama washukiwa.

Da Cunha alipatikana amefariki katika mojawapo ya mali zake mjini Lisbon.

Nuno Ribeiro da Cunha

Chanzo kimoja cha polisi kilikidokeza chombo cha habari cha Portugal kwamba huenda mshukiwa huyo alijiua.

Vyombo vya habari nchini humo vilinukuu polisi wakisema Da Cunha alikuwa tayari amejaribu kujiua mwezi huu na kwamba alikuwa akiugua shinikizo la akili.

Isabel Dos Santos ambaye anakabiliwa na kesi ya ufisadi nchini Angola, mara zote amekuwa akikana mashtaka hayo. Jumatano wiki hii Eurobic ilisema kwamba itasitisha uhusiano wake wa kibiashara na Isabel Dos Santos ambaye ameripotiwa kuwa mwanahisa mkuu wa benki hiyo kupitia kampuni mbili anazomiliki

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles