22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mfanyabishara kizimbani kwa tuhuma za wizi

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

JAMHURI imemfikisha mahakamani mfanyabiashara,, Krushna (37) Mkazi wa Makoroboi Mwanza kwa tuhuma za kuiba bidhaa zenye thamani ya Sh milioni 284.8 alivyopewa na Kiwanda cha Cello kwa madhumuni ya kibiashara.

Mshtakiwa alipanda kizimbani katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Faraji Nguka.

Wakili Nguka anadai mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Mei 19 na Septemba 21, 2018, anadaiwa kuiba  bidhaa mbalimbali

ikiwemo viti, stuli, majagi, vikapu, majaba, ndoo.

Bidhaa zingine ni vifungashio vya chakula,  ndoo za takataka , vikombe na mabeseni, vyote vikiwa na thamani ya Sh 284,845,702 alivyopewa na Kiwanda cha Cello kwa madhumuni ya kibiashara.

Mshtakiwa amekana mashtaka, upelelezi unaendelea na upande wa Jamhuri haukuwa na pingamizi kwa mshtakiwa kupata dhamana.

Hakimu Shaidi ametoa masharti ya dhamana kwamba awe na wadhamini wawili, wenye vitambulisho vya Taifa au taasisi inayotambulika, mmoja asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni moja na mwingine awasilishe hati ya mali isiyohamishika.

Pia mshtakiwa anaweza kuwasilisha fedha taslimu nusu ya jumla ya thamani ya mali anayodaiwa kuibwa.

Mshtakiwa hakufanikiwa kupata dhamana kwa kushindwa kutimiza masharti, kesi iliahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa karudishwa rumande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles