22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara kizimbani kwa kutishia kuua kwa bastola

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MFANYABIASHARA, Adelard Lyakurwa (58) amepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akituhumiwa kumtishia kwa bastola mfanyabiashara maarufu Valence Lekule.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yanayomkabili leo na Wakili wa Serikali, Aziza Mhina mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Martha Mpaze.

Mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kutishia kuua kwa kutumia bastola kinyume na kifungu cha 89 (2)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Mhina anadai Julai 30,2020 maeneo ya Kariakoo mtaa Mbaruku na Swahili wilayani Ilala akiwa na lengo la kuua, alimtishia, Valence Lekule kumuua kwa kutumia bastora huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa Lyakurwa alikana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba ipangiwe tarehe ya kumsomea maelezo ya awali.

Baada ya kusomewa mashtaka, Hakimu Mpaze alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili ambao watakuwa na barua zinazotambulika kisheria na kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni moja.
Mshtakiwa alishindwa kukamilisha masharti hayo na Kesi iliahirisha hadi Juni 2,2021 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles