Mfanyabiashara kizimbani kwa kukutwa na silaha ya moto

0
726

ERICK MUGISHA-DAR ES SALAAM

Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Tandale kwa Tumbo jijini Dar es salaam, Ally Makwaya (40) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto.

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Saada Mohamed, amemsomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mwamini Kazema, akidai Januari 7 mwaka jana eneo la Tandale kwa tumbo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam alikutwa na silaha yenye namba za usajili Uc 49351998 aina ya AK 47.

“Upelelezi wa shauri hili haujakamilika na tunaomba mahakama yako kutoa tarehe nyingine kwa kutajwa na kukamilisha upelelezi” amedai Saada.

Hakimu Kazema amesema mshtakiwa hatoruhusiwa kujibu chochote kwa muujibu wa sheria na kanuni la kosa hadi litakapohamishiwa mahakama kuu.

Amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, mdhamini mmoja awe anafanya kazi kwenye taasisi inayotambulika kisheria,  barua za utambulisho na nakala ya kitambulisho cha Taifa.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Desemba 12 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here