29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara kizimbani kwa kukutwa na bunduki ya kivita

Erick Mugisha -Dar esw salaam

MFANYABIASHARA ambaye ni Mkazi wa Tandale kwa Tumbo, Ally Makwaya (40) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto.

Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Saada Mohamed,  akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mwamini Kazema, alidai Januari 7, 2018 eneo la Tandale kwa Tumbo wilayani Kinondoni,  Dar es Salaam mtuhumiwa alikutwa na silaha yenye namba za usajili Uc 49351998 aina ya AK 47.

“Upelelezi wa shauri hili haujakamilika na tunaomba mahakama yako kutoa tarehe nyingine kwa kutajwa na kukamilisha upelelezi,” alidai Saada.

Hakimu Kazema alisema mshtakiwa hataruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo hadi shauri lake litakapohamishiwa Mahakama Kuu.

Alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, mdhamini mmoja awe anafanya kazi taasisi inayotambulika kisheria,  barua za utambulisho na nakala ya kitambulisho cha taifa.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Desemba 12.

Wakati huo huo, watu wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni Christopher Douglas (24), mkazi wa Mbezi Kimara na Gadi Daudi (27), mkazi wa Makoka Mwisho.

Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Doroce Massawe  akiwasomea washtakiwa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu John Chacha, alidai Novemba 26, 2018 eneo la Mwananyamala wilayani Kinondoni, Dar es Salaam waliiba simu aina ya Samsung Note 4 yenye thamani ya Sh 200,000 fedha taslimu Sh 20,000 na vitenge nane vyenye thamani ya Sh 95,000 mali ya Omary Kibalati,  kabla na baada walimtishia kwa panga ili kujipatia mali hizo.

Washtakiwa wote walikana kutenda kosa na Massawe alidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba mahakama tarehe nyingine kwa kuanza hoja za awali.

Hakimu Chacha alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za kosa washtakiwa hawatakuwa na dhamana, watakuwa wakitokea rumande hadi mwisho na kesi itakuja kwa kuanza hoja za awali Desemba 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles