24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabashara Seth avunja ukimya Mahakamani

KULWA MZEE,DAR ES SALAAM

Mfanyabiashara , Kigogo wa IPTL, Herbinder Seth anayekabiliwa kesi ya uhujumu uchumi amewalalamikia askari magereza kwa kumzuia kuonana na wakili wake kwa miezi Sita sasa.

Seth aliwasilisha malalamiko yake leo Mei 23 na kuomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imruhusu kuonana na wakili wake aliyemtaja kwa jina moja la Mtema kwa sababu amekuwa akizuiliwa kumuona kwa miezi Sita sasa.

Seth aliwasilisha maombi hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, ambapo aliomba kuonana naye ili ampe maelekezo kuhusu kesi hiyo.

Baada ya kutoa malalamiko hayo, Hakimu aliamuru askari magereza kuruhusu mshtakiwa huyo kuonana na wakili wake kwani ni haki yake.

Katika hatua nyingine Wakili wa Serikali, Wankyo Simoni, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutaja shauri hilo ambapo ilipangwa Juni 10 mwaka huu.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalila.

Washtakiwa wamesota rumande tangu Juni 19,2017 walipofikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Seth na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles