27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mfamasia kortini tuhuma za kuiba chupa 30 za ARVs

Abdallah Amiri, Igunga

JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, limemfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Igunga, mfamasia Francis Mlesa (33), anayefanya kazi  hospitali ya wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya wizi wa dawa za wagonjwa.

Awali mwendesha Mashtaka wa Polisi Wilaya ya Igunga, Joseph Mwambwalu aliiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi kuwa mshtakiwa anakabiliwa na shitaka moja la wizi.

Alisema Desemba 24, mwaka jana, saa 1:30 siku katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mshtakiwa Francis Mlesa (33) akiwa mwajiliwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, mfamasia anatuhumiwa kuiba chupa 30 za vidonge vya dawa ya ARVs zote zikiwa na thamani ya 211,600

Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa, mshtakiwa akitambua ni mtumishi wa umma alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 270 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo, alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 31/20 na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh 300,000.

Itakumbukwa Ofisa Tarafa ya Igunga, Shadrack Kalekayo alisema Mlesa alishitukiwa na mlinzi aliyekuwa zamu ya saa 1:30 usiku, baada ya kumuona akiwa amefunga maboksi mawili ya dawa kwenye baiskeli yake.

Alisema baada ya kumuona alimsimamisha na kuanza kumhoji, lakini mtuhumiwa alisema muda wa matumizi wa dawa hizo umepita.

Mlinzi huyo, Rushinangeme Paulo alisema baada kuangalia kwa makini dawa hizo muda wake wa matumizi ulikuwa haujapita.

“Baada ya kumuona anatoka na baiskeli, huku akiwa amefunga maboksi mawili, nilimtilia shaka, nikamsimamisha kumhoji.

“Akanijibu dawa hizi muda wake wa matumizi umekwisha, nilipoziona niliona mbona bado hata mwaka wa kuisha matumizi haujafika,”alisema.

Alisema baada ya kumbana sawa sawa, mtuhumiwa alikimbia na dawa hizo.

Alisema baada ya msako mkali, Desemba 26, mwaka huu walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mbele ya uongozi wa hospitali na kukiri kuiba dawa hizo.

Alisema wakati anahojiwa, alisema alichukua dawa hizo kwa ajili ya kuziteketeza kwa moto kwa sababu zilikuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu tena.

Alisema baada ya kikao hicho, uongozi wa hospitali ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Igunga, Deus Rutha walimpeleka mtuhumiwa kituo cha polisi Igunga.

Mmoja wa mashuhuda, Kasembe Nangale alisema siku tukio alikuwa anatoka kumwangalia dada yake, Chaula Nangale ambaye amelazwa wodi namba 3 akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua, tumbo na mgongo.

Alipofungua ndipo dawa hizo zikaonekana ni ARVs, huku mtumishi huyo akitoroka nazo, baada ya mlinzi kuzidiwa na watu wanaopita katika geti hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles