30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MFALME WA SAUDIA ALIPOZURU INDONESIA KWA NDEGE YA DHAHABU

ILIKUWA ziara ya kihistoria, ziara ya maajabu iliyojaa mbwembwe, madoido, ufahari na utukufu na kubwa kuliko yote unaweza sema kufuru, wakati Mfalme Salman bin Abdul wa Saudi Arabia alipotua Indonesia kwa ziara ya siku tisa kuanzia Machi Mosi mwaka huu.

Alishuka kutoka ndege iliyopakwa dhahabu kwa kutumia eskaleta ya dhahabu kwenye uwanja wa ndege wa Halim Jakarta.

Waliokuwa wakimsubiri kumpokea kwenye njia za ndege ni Rais wa Indonesia Joko Widodo pamoja na gwaride la heshima.

Walielekea makazi ya kirais huko Bogor wakisaidiwa kukingiwa wasilowane mvua kwa miavuli.

Ziara hiyo ya siku tisa, inahusisha siku tatu za kikazi na sita za mapumziko, ambapo mfalme na msafara wake watafurahia maisha mjini Bali, ambako walinzi 100 walimlinda kisiwani hapo huku ziara nzima ikihusisha makomando 10,000 wa Indonesia na Saudia.

Mfalme Salman (81) hakusafiri pekee bali alisindikizwa na ujumbe wa watu karibu 1,500 wakiwamo watumishi 620 na ujumbe wa kiserikali na kibiashara 800.

Ujumbe huo mzito ulioohusisha mwana mfalme 25 ulitua nchini humo kwa ndege saba na kufikia katika hoteli nne za kifahari;The Westin Jakarta, Raffles Hotel Jakarta, Ritz-Carlton Jakarta Mega Kuningan na JW Marriott.

Katika Hoteli ya Westin Jakarta, msafara wake ulikodi vyumba 200.Wakati akiwa katika Msikiti wa Istiqlal, mjini Jakarta lift maalumu iliwekwa na kujengewa choo kipya. Lift hiyo ililenga kumsafirisha mfalme kutoka ghorofa moja hadi nyingine hasa ile ya pili ambako aliendesha maaombi maalumu ya Sunnah.

Ziara hiyo iliashiria mwanzo mpya baina ya mataifa hayo, maana ni mara ya kwanza kipindi cha nusu karne kwa mtawala wa Kifalme wa Saudia kuitembelea Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani.

Mara ya mwisho mfalme wa Saudia kuzuru Jakarta ilikuwa mwaka 1970, wakati Mfalme Faisal bin Abdulaziz Al Saud alipoitembelea nchi hiyo.

Mfalme Salman alikuwa katika ziara ya nchi za Asia wiki mbili zilizopita ikilenga kujenga uhusiano wa Saudia katika eneo hilo.

Alikuwa tayari ameitembelea Malaysia na baada ya kutoka Bali alielekea Brunei, Japan, China na visiwa vya Maldives.

Kama ilivyotarajiwa hakupanda wala kutelemkia kutoka katika ngazi bali eskaleta mbili za dhahabu zilimfuata kote alikokwenda nchini Indonesia.

Ngazi hizo za umeme zinazotumika katika majengo, ziliungana na limo mbili za Mercedes-Benz S600, mizigo binafsi ya tani 459.

Kampuni ya mizigo ya Adji Gunawan iliyopewa jukumu la kushughulika na mizigo hiyo iliandaa wafanyakazi 572 kwa ajili ya mizigo yake hiyo.

Mfalme Salman pia anakumbukwa kwa kufunga ufukwe mzima wa Ufaransa wakati yeye na ujumbe wake walipozuru mji mdogo wa French Riviera mwaka jana.

Ziara yake hiyo ya mapumziko iliwakera wakazi wa mji huo na kilichoonekana kufuru zaidi ni kutandika lift ndefu kutoka hoteli mwaka hadi ufukweni.

Katika mapumziko hayo ya Ufaransa alisafiri na kundi la watui 1,000 wakiwamo wanafamilia na marafiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles