23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mfalme wa Morocco kutua na watu 1,000

MFALME wa Morocco, Mohammed VI
MFALME wa Morocco, Mohammed VI

Na HADIA KHAMIS-DAR ES SALAAM

MFALME wa Morocco, Mohammed VI, anatarajiwa kuwasili hapa nchini kesho huku akiongoza ujumbe wa watu 1,000.

Mfalme huyo anatarajiwa kuwasili saa 10 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema ujumbe huo utakuja na ndege sita kubwa aina ya Boil na ndege ndogo mbili kwa ajili ya shughuli za utalii.

Alisema ujio wa wageni huo utaisaidia nchi kuingiza mapato katika utalii.

“Rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wawekezaji wanakuja nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi,” alisema Makonda.

Pia alisema mfalme huyo anatarajiwa kusaini mikataba 11 ya kiuchumi na utalii.

Alisema mikataba atakayosaini ni pamoja na wakulima wadogo wadogo, masuala ya siasa, masuala ya utalii, nishati na madini, uhusiano wa kimataifa, mifugo na uvuvi na pembejeo za kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles