30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MFALME WA MOROCCO AANZA KUTEKELEZA AHADI YA UWANJA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amekutana na ujumbe wa wataalamu kutoka nchini Morocco ambao watajenga uwanja wa kisasa wa michezo mkoani hapa.

Ujumbe huo wa wataalamu umejumuisha wahandisi, wasanifu wa majengo na wataalamu wa udongo, umetokana na ziara ya Mfalme Mohamed wa 6 wa Morocco aliomuahidi Rais Dk. John Magufuli.

Pia ujumbe huo  ulitembelea eneo la Nzuguni mkoani hapa sehemu  utakapojengwa uwanja huo wa kisasa.

Awali kabla ya kutembelea eneo hilo, ujumbe huo ulikutana na Waziri Dk. Mwakyembe jana ofisi kwake mjini hapa.

Waziri Dk. Mwakyembe alisema serikali imetenga zaidi ya Sh. bilioni moja katika bajeti yake ya mwaka 2017-2018 kwa ajili ya kuanza mchakato wa ujenzi katika eneo hilo.

“Namshukuru Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuikumbuka sekta ya michezo, ile ndoto ya kuwa na uwanja wa kisasa wa mpira sasa imetimia, wengi wanafikiri ni uwanja wa mpira wa miguu pekee, hapana hilo litakuwa eneo changamani la kisasa ambalo litakuwa na michezo ya aina zote, hoteli za kisasa na eneo la maduka makubwa,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema awali walipata eneo kubwa katika eneo la Nala nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, ambapo waliomba ekari 150 na zote walipewa.

Alisema baada ya kupata eneo, Rais aliona eneo hilo si rafiki kutoka na umbali wa kutoka Dodoma mjini hadi Nala, hivyo kuamua   kubadilisha eneo ambapo hivi sasa utajengwa katika eneo la Nzuguni mjini hapa.

Waziri Dk. Mwakyembe pia alimshukuru, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kutenga eneo la ekari 300 katika eneo la Nzuguni kwa ajili ya ujenzi wa eneo changamani la michezo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles