29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

MEYA UBUNGO AWAKUMBUKA YATIMA

MEYA wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob
MEYA wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob

NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

MEYA wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, ametoa zawadi za sikukuu kwa makundi mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni mbili.

Zawadi hizo zilisambazwa katika vituo vya yatima, watu wasiojiweza na viongozi wa mashina wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Dar es Salaam jana katika Kituo cha Yatima cha Ijanga Zaidia, Jacob, alisema zawadi hizo zimetolewa ili kusaidia makundi hayo kusherehekea sikukuu kwa furaha kama ilivyo kwa familia nyingine.

“Huu ni mwisho wa mwaka na mimi ni kiongozi, lazima nionyeshe mfano, siwezi kukaa nyumbani kwangu nafurahia sikukuu na kuwasahau watu walio katika makundi maalumu pamoja na viongozi waliochangia kupata nafasi hii,” alisema Jacob.

Alisema zawadi alizokabidhi ni mbuzi watano, kilo 200 za mchele, juisi na gunia moja la viazi mbatata.

Naye Mkuu wa Kituo cha Ijanga Zaidia, Mussa Sadiki, alisema zawadi hiyo ni msaada mkubwa kwa kituo hicho katika kipindi hiki cha sikukuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles