27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Meya mpya Dar kupatikana Jumamosi

MAKWEMBENA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

UCHAGUZI wa kumpata meya wa Jiji la Dar es Salaam atakayemrithi Dk. Didas Masaburi unatarajiwa kufanyika Januari 23, mwaka huu.

Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Gaston Makwembe, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika.

“Tupo katika maandalizi ya kuhakikisha meya wa jiji anapatikana katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii, na vyama vyote tunatarajia kuvitumia barua ya mwaliko muda si mrefu,” alisema Makwembe.

Alisema uchaguzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Karimjee, huku akisisitiza kuwa vyama vyote vyenye uwakilishi wa madiwani katika jiji hilo vitashiriki.

Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mvutano wa aina yake kati ya vyama vinavyounda na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo, Ukawa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ambapo wanaizidi CCM kwa jumla ya madiwani 13.

Iwapo Ukawa watafanikiwa kutwaa jiji hilo, itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa wapinzani kuongozakuliongoza tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alitoa wito kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia uchaguzi huo kwa amani na haki.

“Uchaguzi huu wa meya wa jiji usifanyike kama ule wa kumtafuta meya wa Ilala na Kinondoni uliokuwa na mizengwe mingi iliyochangiwa na CCM kutokubali kushindwa na wapinzani,” alisema Makene.

Diwani wa Kata ya Vijibweni, Isaya Mwita (Chadema) ndiye atapeperusha bendera ya Ukawa huku mgombea wa nafasi ya naibu meya akitarajiwa kutoka chama cha CUF.

CCM YATEGEMEA MUUJIZA

Akizungumzia uchaguzi huo, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abillahi Mihewa, alisema kuwa licha ya uchache wao lakini inaweza kutokea miujiza ya Mwenyezi Mungu wakaibuka washindi kwa kumpata meya. Watawakilishwa na Diwani wa Kinondoni, Yusuph Omary Yenga.

“Unajua Mwenyezi Mungu ni mkubwa, pamoja na wingi wao wanaweza kuamka wakaongozwa na maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba ‘rais anaweza kutoka chama chochote lakini rais bora atatoka CCM’, na inaweza kuwa hivyo kwa meya,” alisema Yenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles