24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Iringa akalia kuti kavu

Raymond Minja -Iringa

MEYA wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (Chadema), amekalia kuti

kavu linalohatarisha nafasi yake kabla ya muda wake kumalizika miezi mitatu ijayo.

Zikiwa zimesalia siku 90, madiwani wa halmashauri hiyo wamemtuhumu kwa makosa kadha katika makundi manne ambayo yanaweza kusababisha

apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.

Barua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Ahamed Njovu iliyoandikwa kwenda kwa meya huyo na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana, imetaja makosa kuwa ni pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.

Pia anatuhumiwa kufanya matumizi bila

kuzingatia kanuni za kudumu za halmashauri, kinyume na taratibu na

aliamuru baadhi ya wajumbe wa halmashauri kufanya ziara mikoa

ya Njombe na Mbeya pasipo mkuu wa mkoa kujiridhisha kinyume na kanuni

za kudumu za halmashauri.

Aidha anahusishwa na kugawa nafasi za kamati kwa upendeleo kwa kigezo cha tofauti za kisiasa na chuki binafsi na anadaiwa kumiliki mali zisizoendana na kipato chake

Pia anadaiwa kujipatia tenda za kufanya kazi za halmashauri kwa kutumia majina ya rafiki zake wa karibu wenye kampuni za kandarasi.

Kosa la pili, ni matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri, ikiwa ni pamoja na kutumia gari kwa kazi binafsi kinyume na kanuni za halmashauri.

Katika kosa la tatu, anatuhumiwa kuwa na mwenendo mbaya na ukosefu wa nidhamu.

 Kosa la nne, anatuhumiwa kushiriki vitendo vya rushwa katika ofisi yake jambo ambalo haliendani na kanuni

za halmashauri.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,

amekiri kupokea maombi yaliyosainiwa na wajumbe 19 wa halmashauri

yakitaka kufanyika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kujadili kumwondoa madarakani.

Kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za mwaka 2015, kifungu namba 5, kifungu kidogo cha 2 hadi 7, kinaagiza baada ya mtuhumiwa kupokea maombi ya tuhuma zinazomkabili, anatakiwa kuwasilisha majibu yake ndani ya siku tano.

Baada ya kupokea utetezi, mkurugenzi alisema atamwarifu mkuu wa mkoa

tuhuma zinazomkabili meya pamoja na utetezi wake ili kuzipitia.

“Baada ya mkuu wa mkoa kupokea taarifa, ataunda timu ya uchunguzi

ya kushughulikia tuhuma hizo na timu hiyo baada ya kukamilisha kazi

yake na kuwasilisha taarifa yake, mkuu wa mkoa atawasilisha taarifa

kwa mkurugenzi wa manispaa,” alisema.

Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, ndani ya siku 14, mkurugenzi atawasilisha kwenye Baraza la Madiwani kwa uamuzi wa tuhuma zinazomkabili muhusika.

Alipoulizwa kuhusu sakata hilo, Kimbe alikiri kupokea barua yenye tuhuma hizo na akaahidi kutoa ufafanuzi wake katika kikao alichotarajia kufanya na waandishi wa habari jana jioni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles