30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Ilala awataka wanawake kuwekeza

Tunu Nassor -Dar es Salaam

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wanawake wa halmashauri hiyo kujikita katika uwekezaji ili kujikwamua kwenye hali ngumu na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo aliyasema jana Dar es Salaam, wakati akifunga mafunzo ya wanawake na vijana wajasiriamali wa Kata ya Gongo la mboto yalioandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo.

“Napenda kumshukuru Mwenyekiti wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo, Neema Mchau, kwa juhudi zake za kuisaidia Serikali, hasa wilayani Ilala kwani amewainua wanawake katika shughuli za uzalishaji, amewapatia ujuzi, sasa wanamiliki viwanda vyao,” alisema Kumbilamboto.

Alisema sasa ni wakati wa wanawake kusimama imara katika viwanda vidogo vidogo ambavyo vinazalisha bidhaa na kuzitangaza katika masoko ya ndani na nje.

Kumbilamoto alisema Serikali mwaka huu inakabidhiwa soko la kisasa la Kisutu ambalo ujenzi wake umegharimu Sh bilioni 13, litakapoanza kutumika soko hilo watawekwa wafanyabiashara wa awali na nafasi za wafanyabiashara 700.

Pia ameitaka taasisi hiyo na wafanyabiashara kuchangamkia fursa kwani soko hilo litakuwa la kisasa na watalii watafikia hapo na ndio mradi mkubwa wa soko la kipekee Ilala.

Amewataka wananchi wa Ilala kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kukuza uchumi wa viwanda. 

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inatoa mikopo ambayo haina riba kupitia halmashauri kwa vikundi vinavyotambulika, hivyo wakopaji wakope fedha hizo na wakumbuke marejesho ili wengine nao waweze kukopa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Fahari Tuamke Maendeleo, Neema alimpongeza Meya Kumbilamoto ambaye ni mlezi wa taasisi hiyo.

Alisema mafunzo hayo yalikuwa ya wiki moja ya utengezaji sabuni, mafuta ya kupaka na sabuni za maji na kila mshiriki amepewa cheti cha ushiriki kwa kufanya vizuri.

Neema alisema kwa sasa anamiliki kiwanda chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles