26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA ILALA AONGOZA WANANCHI UPIMAJI MACHO

NA VERONICA ROMWALD- DAR ES SALAAM


MEYA wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, amewaongoza wakazi zaidi ya 600 wa   Buyuni na Chanika   kupima afya ya macho na shinikizo la damu.

Upimaji huo uliofanyika jana katika viwanja vya Shule ya  Msingi Buyuni ulitekelezwa  na Klabu ya Lion na Benki ya DTB.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika upimaji huo, Meya Kuyeko alisema ni muhimu wananchi wawe wanachunguza afya zao mara kwa mara.

“Hasa afya ya macho ni muhimu maana mtu ukiwa kipofu ni matatizo makubwa, unakuwa unatembea kifo kipo mkononi, utahitaji uangalizi wa karibu hata kama utakuwa na uwezo wa kufanya baadhi ya vitu mwenyewe,” alisema.

Aliipongeza klabu hiyo kufanya upimaji huo huku akitoa wito kwa wadau wengine wa afya kuiga mfano huo.

 Gavana wa Klabu hiyo aliyemaliza muda wake, Abdul Majee Khan, alisema upimaji huo wa macho na shinikizo la damu ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa Klabu ya Lion.

“Kila mwaka tumekuwa tukifanya upimaji kwa sababu matatizo ya upofu yanazidi kuongezeka duniani.

“Inakadiriwa takriban watu milioni 40 wanaogua na ifikapo 2020 idadi hiyo huenda itaongezeka mara mbili yake hadi milioni 80 iwapo hatua hazitachukuliwa,” alisema.

Alisema mwaka jana pekee katika eneo hilo walipima watu zaidi ya 600 kati yao 450 walipatiwa miwani za kusomea na wengine walipatiwa matibabu ya macho.

“Na leo (jana) watakaokutwa wana matatizo tunawasaidia kuwapa miwani   na matibabu bila kulipia gharama yoyote.

“Na wale ambao huhitaji upasuaji wa kuondoa mtoto wa jicho huwa tunawahamishia katika hospitali za rufaa na tunagharamia matibabu yao pia,” alisema.

Alisema chama hicho kinafanya kampeni za upimaji magonjwa mengine ikiwamo kisukari,  upasuaji wa moyo, kampeni ya surua na rubella.

“Tunasaidia walemavu, watoto yatima, upandaji miti na majanga mengine yanayojitokeza kutokana na athari za mvua,”  alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles