31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 24, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Dar awafunda madiwani

issaya-mwitaNA HADIA KHAMIS

-DAR ES SALAAM

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amewataka madiwani kuhamasisha wananchi washiriki katika shughuli za uchangiaji maendeleo ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa badala ya kuisubiri Serikali.

Alikuwa akizungumza mwishoni mwa wiki   katika  mahafali ya darasa la saba katika shule ya Msingi Mbezi Luisi.

Mwita alisema licha ya Serikali kutangaza utoaji wa elimu bure bado Watanzania wana wajibu kushiriki kwa ukamilifu kwa kuweka miundombinu bora.

Alisema madiwani kwa kushirikiana na viongozi wa kamati za uongozi za shule wanatakiwa kuweka mikakati  wanapoona shule ina upungufu wa vyumba na mahitaji mengine badala ya kusubiri Serikali kutatua changamoto hiyo .

“Elimu ni bure sawa, lakini Madiwani fanyeni kazi yenu kama viongozi ambao mmechaguliwa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi wenu.

“Hamasisheni watu na nyie wazazi kamati ya shule inaposema jambo jitahidini kutenda ili yale ambayo tumekusudia kuyafanya tuonyesheni ushirikiano,” alisema Mwita.

Alisema madiwani wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanashirikiana na Serikali   wananchi wapate maendeleo yaliyokusudiwa na kwa wakati.

“Wote tunatakiwa kuijenga nchi yetu kwa kuwa ndiyo watu pekee ambao wanaweza kufanya haya, lakini kama madiwani ambao ndiyo mpo muda mwingi na wananchi mtashindwa kufanya juhudi za kuleta maendeleo hakutakuwa na sababu ya nyie kuwapo,” alisema.

Diwani wa Kata ya Mbezi,  Humphrey Sambo (Chadema), alisema kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ni ya wananchi wote na   atahakikisha wanashrikiana na viongozi wa shule  kumaliza haraka ujenzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles