23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA DAR AONYA UNYANYASAJI KWA WAJANE

Na TUNU NASSOR–DAR ES SALAM


MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, ameonya tabia ya unyanyasaji dhidi ya wajane unaofanywa na baadhi ya wanafamilia pindi mume anapofariki.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa ibada  ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Ukonga, marehemu Leornad Lukala iliyofanyika katika Mtaa wa Mongolandege.

Alisema hivi sasa familia nyingi zimekuwa na dhana potofu ya kuwanyanyasa wajane huku ndugu wa familia wakidiriki kuwadhulumu mali jambo ambalo huwafanya kuishi katika  mazingira magumu na upweke.

Mwita alisema jambo hilo halikubaliki wala kuvumilika katika jamii ya kitanzania na hivyo kumtaka kila mmoja kuchukua tahadhari .

“Kumekuwa na tabia ya watu kunyanyasa wajane, hawa watu walioondokewa na wenzi wao …familia zimekuwa na sauti badala ya mfiwa, wanadhulumu mali, jambo linalosababisha kuongezeka kwa kesi za mirathi mahakamani.

 “Niwaombe sana, wajane wasitengwe, wapewe huduma zao kama ilivyokuwa awali, msifanye watu hawa wakajutia kubaki duniani, msitumie nafasi zenu kuwadhalilisha, wapeni huduma kama wengine,” alisema Mwita.

Alisema kuwa dhuruma na kuwatenga wajane ni jambo ambalo limekuwa likiwatesa na kusababisha kushitaki.

Katika hatua nyingine Meya Isaya, aliwataka viongozi mbalimbali waliopewa nafasi za kuhudumia wananchi wanapaswa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuacha alama pindi wanapomaliza muda wao.

“Naomba sana viongoziambao tumepata nafasi za kuwatumikia wananchi, iwe ni kwenye sekta ya dini, kisiasa, serikalini, na sehemu nyingine, tujitahidi kutekeleza majukumu yetu kikamilifu ili tunapoondoka duniani tuache kumbukumbukwa vizazi vijavyo,” alisema.

Mchungaji Lukala alifariki dunia juzi alipokuwa akipelekwa kwenye kituo cha afya cha Mongolandege ambapo atazikwa leo kijijini kwao Mwanalumango Kisarawe mkoani Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles