25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mexime, Yanga hakijaeleweka

Theresia Gasper – Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema bado hajamalizana na Yanga ambayo inamwitaji  kwa ajili ya  kuwa kocha msaidizi wa Mbelgiji, Luc  Eymael.

Kwa muda mrefu Yanga imekuwa ikitamani kufanya kazi na Mexime, lakini imekuwa ikikwama kutokana na pande hizo mbili kutoafikiana.

Yanga sasa inafundishwa na Eymael ambaye alirithi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, aliyefungashiwa virago kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi hicho cha Jangwani.

Eymael anasaidiwa na Charles Mkwasa ambaye kabla ya ujio wa mzungu huo alikuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu.

Mkwasa hata hivyo hajathibitishwa rasmi na uongozi wa klabu hiyo kushika wadhifa huo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mexime alisema uongozi wa Yanga bado haujakamilisha taratibu za kung’oa Klabu ya Kagera Sugar anayoifundisha kwwa sasa, licha ya kwamba mazunguzo yanaendelea.

“Naendelea na majukumu ya timu yangu kama kawaida kuhusu Yanga bado hawakamilisha taratibu zozote hadi sasa, ila mimi nawasubiri wao kwa sasa anaendelea na majukumu mengine Kagara,” alisema.

Alisema kwa sasa anaendelea kukinoa kikosi chake ili kiwe na ushindani mkubwa na kufanya vizuri katika mechi zinazowakabili mbele yao.

Mexime alisema baada ya kuona baadhi ya mapungufu kwenye timu yake anaendelea kuyafanyia kazi ili yasiendelee kujitokeza katika mechi nyingine.

Kocha huyo alisema usipokuwa makini unaweza ukapoteza mechi kirahiai na mipango yao ni kuendeleza ushindi kama walivyofanya katika mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles