23 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Metacha ajutia makosa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kipa wa Yanga, Metacha Mnata, amewaomba radhi Wanayanga na wadau wa soko kwa kitendo alichofanya jana baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huoa mabao Yanga ilishinda mabao 3-2, Metacha alionesha ishara ya matusi mashabiki walikuwa wakimzomea.

“Kwa niaba ya familia yangu, management yangu na mimi mwenyewe napenda kuchukua fulsa hii kuomba msamaha kwa viongozi wa klabu yangu ya Yanga SC, wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, mashabiki wa klabu ya Yanga, mamlaka za soka nchini na wadau wote wa soka ambao wamekwazika kwa kwa kitendo nilichokifanya jana.

“Nikiri hakikuwa kitendo cha kiungwana hivyo najutia makosa niliyoyafanya. Mimi kama mchezaji wa Yanga na timu ya Taifa napaswa kuwa mfano mzuri siku zote mbele za watoto na wanaotamani kuwa kama mimi na watu ambao aidha walikuwepo kiwanjani au waliona mechi kupitia televisheni majumbani kwao.

“Natambua mchango na umuhimu wa mashabiki kwangu binafsi na kwa klabu, hivyo kitendo kile hakikupaswa kutokea,” ameandika Metacha katika ukurasa wake wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles