24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MESSI, SUAREZ WAMPIGIA GOTI NEYMAR

BARCELONA, Hispania


KLABU ya Barcelona imedhamiria kumbakisha nyota wake, Neymar Jr, kwa kuwatumia nyota wake; Lionel Messi, Luis Suarez na Gerard Pique, kujaribu kumshawishi nyota huyo kukataa ofa ya Paris Saint Germain (PSG).

PSG wameahidi kutoa pauni milioni 196 na mshahara wa pauni 500,000 baada ya makato ya kodi kwa wiki kwa nyota huyo wa zamani wa Santos.

Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Bartomeu, alijaribu na kushindwa kumzuia Neymar asijiunge na miamba hiyo ya Ufaransa kabla ya kuwatumia wachezaji wenzake kumwomba akatae ofa hiyo.

Messi na Suarez tayari wamewasilisha maoni yao kwa Neymar wakiwa katika maandalizi jijini New Jersey huku wakiungana na Pique katika jambo hilo.

Hata hivyo, Bartomeu alieleza kuendelea na ushawishi dhidi ya nyota huyo ambaye anaweza kuachana na klabu hiyo.

Mtandao wa Marca wa nchini Hispania ulieleza kuwa endapo PSG itamsajili  nyota huyo, inaweza kukutana na rungu la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) katika matumizi ya fedha.

Barcelona pia wanajaribu kutafuta saini ya nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho kwa pauni milioni 80 kwa madai ya ukaribu wake na Neymar.

Wakati huo huo, kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ameonekana kufurahia kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata na kueleza mara zote Mhispania huyo alikuwa chaguo lao la kwanza.

Aidha, Conte amemtaka Morata kuthibitisha thamani yake na kusisitiza kuwa ndiye aliyekuwa chaguo lake la kwanza licha ya kwamba pia alimtaka Romelu Lukaku.

Conte alisema: “Huu ni usajili mzuri kwetu. Morata ni mchezaji kinda lakini ana uzoefu mkubwa na nyuma aliichezea Real Madrid na Juventus na ana uzoefu mkubwa kwenye ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bado  ni mdogo na anaweza kujizatiti sana. Huu ni usajili mzuri kwetu.

“Kwa uhakika soko hili la usajili ni la kuchanganya, lakini si kwa msimu huu tu, ila sasa kuna fedha za kuchanganya. Kama unataka kununua mchezaji rahisi, mchezaji wa kawaida unayeanza kumfikiria utatumia euro milioni 40-50.

“Hali hii ni ya kushangaza. Lakini kuna hali hii na lazima tuishi katika hilo. Ni sawa. Lukaku amegharimu kiasi kikubwa cha fedha, lakini ni sawa na Lacazette na Arsenal imetumia euro milioni 65.

“Kwa beki mzuri unatumia Euro milioni 60-70. Hii ndiyo hali ilivyo sasa na lazima tuwe wazuri sana na kutofanya makosa wakati unanunua mchezaji. Lazima utumie kiasi kikubwa cha fedha na kuchagua ni muhimu sana.

“Morata ni chaguo letu la kwanza. Ni mshambuliaji mzuri, mchezaji mwenye matarajio sahihi kwa Chelsea. Anaweza kuonyesha thamani yake na sisi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles