Messi, Neymar vitani Kombe la Dunia

0
1096
Neymar da Silva
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Neymar da Silva

BRASILIA, Brazil

WASHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na Neymar da Silva, wameingia katika vita ya ufungaji bora katika fainali za Kombe la Dunia baada ya wote wawili kupachika mabao manne hadi sasa.

Messi alifunga mabao mawili katika ushindi wa Argentina wa mabao 3-2 dhidi ya Nigeria na kufikisha mabao manne sambamba na mshambuliaji wa Brazil, Neymar amepachika mabao manne baada ya kufunga mawili mechi ya ufunguzi dhidi ya Croatia, kisha kuongeza mawili katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Cameroon.

Nyota wengine wanaonyukana kuwania nafasi ya ufungaji bora ni, Arjen Robben, Robin van Persie, James Rodríguez, Enner Valencia, Karim Benzema na Thomas Müller.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here