31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Messi kukata rufaa kifungo chake

Lionel Messi
Lionel Messi

BARCELONA, Hispania

NYOTA wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, anatarajia kukata rufaa ya kifungo chake cha kwenda jela miezi 21 kwa kosa la udanganyifu wakati wa ulipaji kodi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na baba yake wanadaiwa kukwepa kulipa kodi ya mwaka 2007 na 2009, kwa ajili ya matangazo ya picha za mchezaji huyo.

Fedha za matangazo hayo zilikuwa zinakusanywa na baba yake na kuzipeleka mafichoni kwenye visiwa vya Belize na nchini Uruguay ambapo hakuna makato ya kodi.

Kutokana na hali hiyo mchezaji huyo na baba yake walishtakiwa na juzi walihukumiwa kwenda jela miezi 21 na kutakiwa kulipa faini jumla ya pauni milioni 4.9.

Hata hivyo, Sheria za mahakama nchini Hispania, zinasema mshtakiwa ambaye anatakiwa kutumikia jela chini ya miaka miwili anaweza kuwa chini ya uangalizi, hivyo Messi na baba yake wanaweza wasitumikie gerezani wakatumikia kifungo cha nje na kulipa faini hiyo.

Mwanasheria wa mchezaji huyo na baba yake amesema kwamba, wanatarajia kukata rufaa juu ya kesi ya mteja wake.

Mwanasheria huyo amedai watapambana kwa hali na mali kuhakikisha mchezaji huyo anakuwa huru na anaendelea kucheza soka lake.

Kitendo hiki kinaweza kumweka katika wakati mgumu mchezaji huyo hasa kwenye msimu mpya wa ligi, kutokana na ujumbe ambao anaupata mara baada ya kutangaza kujiuzulu kuitumikia timu ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles