27.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Messi awalaza mashabiki Nou Camp

BARCELONA, HISPANIA 

MASHABIKI wa timu ya Barcelona, juzi ilikuwa siku ya pili kukesha kwenye Uwanja wa Nou Camp wakiandamana kumtaka rais wa timu hiyo Josep Bartomeu kujiuzulu kutokana na mshambuliaji wao bora Lionel Messi kutangaza anataka kuondoka.

Mapema wiki hii nyota huyo ambaye ni mchezaji bora duniani akiwa na jumla ya tuzo sita za Ballon d’Or, ametangaza kutaka kuondoka kutokana na mwenendo mbaya wa timu msimu huu akiamini unatokana na uongozi.

Mashabiki pia wanaamini bodi ya timu inayoongozwa na rais huyo ndio chanzo kikubwa cha timu kuwa na matokeo mabaya kama vile kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu pamoja na kupigwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na hali hiyo, Messi ameuambia uongozi kuwa anataka kuondoka wakati huu wa kiangazi, hivyo mashabiki wamekuja juu kwa kuutaka uongozi kujiuzulu kwa kumuacha mchezaji huyo akiondoka.

Mashabiki walianza kuandamana tangu Jumanne kwenye viwanja hivyo vya Nou Camp wakikesha kuimba nyimbo za kumtaka rais na viongozi wake wajiuzulu.

Hata hivyo, walinzi walijitokeza kwa wingi kujaribu kuwazuia, lakini waliwashindwa kutokana na idadi kubwa ya mashabiki.

Mkataba wa rais huyo umebakiwa wa mwaka mmoja, lakini mashabiki wamedai inatosha na huu ni wakati wake wa kufanya maamuzi magumu ya kujiuzulu.

Baada ya Messi kutangaza kutaka kuondoka klabu mbalimbali zimeonesha nia ya kuitaka saini yake, miongoni mwa timu hizo ni pamoja na Manchester City, Manchester United, PSG, Inter Milan na zingine nyingi.

Baba wa mchezaji huyo ameripotiwa kuwa, tayari amewasili jijini Manchester kwa ajili ya kufanya mazungumzo na klabu hizo juu ya uhamisho wake, lakini PSG wanadaiwa kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili kutokana na ushawishi wa nyota wa zamani wa Barcelona, Neymar ambaye anakipiga kwa mabingwa hao wa nchini Ufaransa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,679FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles