22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Messi aikata kauli ya Manuel Neuer

MessiBARCELONA, HISPANIA
SIKU moja kaba ya mchezo wa juzi wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Barcelona dhidi ya Bayern Munich, mlinda mlango wa Bayern, Manuel Neuer, alisema kuwa katika mchezo huo atahakikisha Messi hapati bao.
Neuer alisema, atamuonesha kuwa yeye ni nani katika soka na jinsi anavyoweza kulinda lango kama ilivyokuwa katika mchezo wa fainali Kombe la Dunia mwaka jana.
“Nitamuonesha mimi na yeye nani zaidi, nitahakikisha hapati bao kama ilivyo katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka jana,” alisema Neuer, kabla ya mchezo wa juzi.
Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi ameikata kauli hiyo juzi, baada ya kupachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0.
Haikuwa kazi rahisi kwa mchezaji huyo kuweza kupata bao, lakini kutokana na ubora wake alifanikiwa kutumia vitendo kuweza kumnyamazisha mlinda mlango huyo namba moja wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern.
Messi mbali ya kufunga mabao mawili, lakini alifanikiwa kutoa pasi ya mwisho ambapo mshambuliaje mwenzake, Neymar kupachika bao katika dakika ya 90.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Arsenal, Thierry Henry, amemsifia Messi na kusema kuwa “Hakuna swali juu ya uwezo wa mchezaji huyo kwa kuwa kila siku anaelezewa ubora wake.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles