20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MESSI AENDELEA KUPUNGUZA MAWAZO IBIZA

MADRID, HISPANIA

KUFUATIWA timu ya taifa ya Argentina kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, staa wa timu hiyo na klabu ya Barcelona, Lionel Messi, anaendelea kupunguza mawazo kwenye visiwa vya Ibiza.

Baadhi ya wachezaji wa Barcelona tayari wamejiunga katika klabu hiyo kwa ajili ya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Messi ambaye alikuwa nahodha wa Argentina, alishindwa kuibeba timu hiyo kwenye Kombe la Dunia na kujikuta wakiondolewa katika hatua ya 16 bora dhidi ya mabingwa wa michuano hiyo Ufaransa.

Mchezaji huyo ameonekana kwenye visiwa hivyo akiwa na familia pamoja na rafiki zake wa karibu ambao wamekuwa wakitumia muda wao kwa ajili ya kumfariji.

Messi alikuwa mmoja kati ya wachezaji ambao walikuwa wanaangaliwa na idadi kubwa ya mashabiki duniani hasa katika michuano hiyo nchini Urusi pamoja na staa wa Ureno na klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo.

Ronaldo na Messi ni vinara duniani wa tuzo za Balllon d’Or, huku kila mmoja akichukua mara tano, lakini hadi sasa hawajaweza kubeba Kombe la Dunia katika maisha yao ya soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles