MERKEL AANZA ZIARA AFRIKA

0
721

 

 

DAKAR, SENEGAL


Kansela  wa Ujerumani, Angela Merkel, alianza ziara yake ya siku tatu barani Afrika kituo cha kwanza kikiwa nchini Senegal.

Katika ziara hiyo Merkel anatarajia kuzungumzia kuhusu kukabiliana na wahamiaji haramu.

Akiwa Senegal Kansela Merkel anatarajiwa kukutana na Rais Macky Sall katika mji mkuu Dakar, na baadae kufuatiwa na mikutano na viongozi wa makundi ya jumuiya za kiraia.

Ujumbe wa Merkel unawahusisha pia wataalamu wa masuala ya umeme, mifumo ya kidijitali, miundombinu na usimamizi wa nishati.

Merkel pia atazuru Ghana na Nigeria siku ya Alhamisi na Ijumaa.

Kansela Merkel alisema awali kwamba ziara yake itahusisha pia mazungumzo kuhusu kuanzisha fursa za ajira katika nchi hizo tatu ili kuwazuia watu wake kujaribu kukimbilia Ulaya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here