Meridianbet walipimana nguvu na kikosi cha timu ya wahamasishaji kilichoongozwa na Jemedari Said Kazumari, na Foby wikiendi iliyopita.
Kabla ya mechi hii ya kirafiki, pande hizi mbili zilitambiana kuondoka na ushindi na maandalizi yalifanyika vyema kuhakikisha kila timu inajiweka kwenye nafasi ya ushindi.
Mechi hii iliyobeba dhumuni kubwa la kuwaleta pamoja wahamasishaji na wafanyakazi wa kampuni ya Meridianbet, na kuleta chachu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Mechi ilianza vyema kwa wahamasishaji kutawala mchezo huo, wakiwavujisha jasho wafanyakazi wa Meridianbet ambao walijitahidi kupambana na mchezo huo mgumu. Meridianbet walijitahidi kufurukuta kwa dakika kadhaa lakini haikuwa bahati yao na wahamasishaji wakawagawia dozi na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Kikosi cha Meridianbet, kikiwakilishwa na Twaha Mohammed kutoka kitengo cha masoko, na Sylvester John kutoka kitengo cha uendeshaji wamezungumzia kupoteza mchezo huo ambao walitamba kushinda awali ni kutokana na mazoezi.
“Mchezo ulikuwa mzuri, isipokuwa kwa upande wetu mazoezi ni changamoto kidogo, hivyo tumeshindwa kukimbizana na kasi ya mchezo wa huu.” – Sylvester John.
“Hawa tungeweza kuwafunga hawa, wanaonekana wanafanya mazoezi sana na sisi tutajinoa upya mechi ijayo lazima wakae wao” – Twaha Mohammed
Kwa upande wa wahamasishaji, wanasema hakukuwa na namna kuwa Meridianbet wangeshinda mechi hiyo kwa kuwa wao tayari wana wataalamu.
“Hawa ilikuwa lazima tuwachape tu, maana timu yetu ina wataalamu. Tuna Jemedari, Jackob Mbuya na mimi hapa, pia na mafundi hao wengine, hawa hawawezi kupata ushindi kwetu” Foby
Hata hivyo, pande zote mbili zilipata wasaa wa kuwa pamoja, na kuwa na wakati mzuri ambalo lilikuwa ni lengo kuu la mechi hii ya kirafiki.