Meridianbet wameshirikiana na Polisi, kituo cha Mtongani Police Post Kuboresha muonekano wa kituo hicho kwa kupaka rangi, ikiwa ni moja ya jitihada zao za kurejesha kwa Jamii.
Kampuni ya Meridianbet, ambayo ni Kampuni kongwe zaidi ya ubashiri Tanzania, ambayo ina masoko mengi ya Ubashiri imekuwa ikishiriki shughuli mbali mbali za kijamii. Ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo vya wagonjwa na watu wenye mahitaji maalumu ili kuwashika mkono.
Kwa mujibu wa Afisa kutoka kitengo cha Masoko wa Meridianbet, Twaha Mohamed, Meridianbet wanaendelea kujiweka Karibu zaidi na umma wakiamini usalama wa umma na wateja wao ni jambo la msingi, muonekano mzuri wa kituo cha polisi ni muhimu wakati wao wakishughulikia usalama wa raia na mali zao.
“Ndiyo, sisi kwa upande wetu tumepata hamasa ya kufanya hili, kama ambavyo tunafanya shughuli zingine za kijamii. Kupaka rangi kituo cha polisi ambao wanahusika moja kwa moja na ulinzi wa raia na mali zao ni moja ya shughuli za kuwa Karibu zaidi na Jamii na kuboresha uhusiano na Jamii na wateja wetu.”
Uupande wa polisi, Mkuu wa kituo cha Mtongani, ametoa shukrani zake na kutoa wito kwa makampuni mengine kushirikiana na Jamii kwa mfano wa Meridianbet.
Meridianbet wanaahidi kuwa wataendelea kushirikiana na jamii, na wana mipango ya kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega na jamii katika nyakati zote na nyakati za matatizo.
“Tunaendelea kujitahidi kuwa Karibu sana na Jamii yetu, maana ndiyo wateja wetu walipo na uhalisia pia kuwa tunatakiwa kuwajibika kwa Jamii. Meridianbet katika msoko yake duniani kwote tunafanya jitihada za kuwa Karibu na umma hata wakati wa matatizo kama tulivyojitahidi kwa nafasi yetu mwanzoni mwa covid-19”
Meridianbet wametaja kuwa zoezi hilo lilienda sambamba na uboreshaji wa maduka yao katika eneo la Mtongani, kuwafanya wateja wapate huduma bora zaidi za ubashiri kwa michezo ya kasino na bashiri za michezo.