Meridian BET, Lions Club wawapiga tafu wazee Kinyerezi

KAMPUNI ya Mchezo wa Kubahatisha ya Meridian Bet, Lions Club na Kituo cha Jamii cha Tiba ‘CCP Medicine’, wameandaa mradi wa kusaidia wazee hapa nchini utakaotekelezwa kwa miaka mitano kuanzia sasa.

Jumapili ya Septemba 20, 2020, Meridian Bet na Lions Club, ilitoa misaada ya vyakula kwa wazee wanaoishi Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa misadaa hiyo ni unga, mchele, chumvi na mito.

Msaada huo ni katika kuunga mkono juhudi za kuwasaidia wazee kuelekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi ya kila mwaka.

Amani Siaforo Maeda kutoka Meridian Bet, alisema: “Tumeanza kwa kutoa hivi leo, itakuwa mwendelezo na tutakuwa tukitoa kwa wazee mbalimbali.”

Naye Mratibu wa Lions Club, Rizwan Kadri, alisema kwa kushirikiana na Meridian Bet, wameamua kuwashika mkono wazee na kuwatia faraja kupitia misaada hiyo.

Dokta Manase kutoka CCP Medicine, aliwashukuru Meridian Bet na Lions Club kwa kusema: “Tunawashukuru Meridian Bet na Lions Club kwa kutoa muda wao ili kushiriki katika kuwafariji wazee wetu kwa kuwapatia mahitaji muhimu ambayo yataweza kufariji katika maisha yao.

“Kutokana na utafiti tulioufanya, tumekusudia kutokomeza matatizo ya kiafya yawapatayo wazee kiafya, kisaikolojia, kihisia na kiroho ili kuwaboreshea maisha yao.

“Wazee wanahitaji malezi, makazi bora, afya bora na mawasiliano mazuri. Tunatoa tiba za aina mbalimbali kama vile tiba ya kisaikolojia, kisanaa, kimuziki na tiba ya lishe itakanayo na wanyama na mimea ambayo imeonesha matokeo chanya ya kuponesha ukilinganisha na dawa.

10 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here