27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Meridiabet yazipa vifaa timu zote kwenye bonanza la street soccer

Kampuni maarufu ya kubashiri matokeo ya Meridianbet imetoa vifaa vya michezo kwa timu zote zilizoshiriki bonanza la soka la timu za mtaani lililopewa jina la Meridian soccer street bonanza lililofanyika leo kwenye viwanja vya Fire, Dar es Salaam.

Afisa masoko wa Meridianbet, Twaha Ibrahim amezikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni seti za jezi na mipira timu za Kigambo Fc ambayo ilikuwa bingwa, Pemaco Fc ya Mbezi Beach iliyokamata nafasi ya pili, Northern Boyz ya Mbagara na Matombo FC ya Upanga na kubainisha moja ya mkakati wa kampuni hiyo hiyo ni kusapoti timu za mtaani ambazo baadhi ya wachezaji wake ni wateja wao.

Twaha ambaye aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa Meridianbet amesema hamasa iliyoonekana kwenye bonanza la leo limethibitisha namna vijana wengi wana vipaji lakini hawapati nafasi ya kuonekana.

Katika bonanza hilo, Kigamboni FC ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa
Pemaco mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliokuwa na amsha amsha kwa mashabiki wa pande zote mbili.

Babi Nyanda ndiye alikuwa shujaa wa Kigamboni baada ya kufunga mabao mawili pekee na jingine likifungwa na Salum Chubi na timu hiyo kuondoka na seti ya jezi na mipira miwili huku Gerald Gerald ‘Samatta’ na Baina Juma wakifunga yale ya Pemaco na kumaliza wa pili wakiondoka na seti ya jezi na mpira mmoja.

Northern Boys walimaliza wa tatu na kuzawadiwa seti ya jezi na Matombo FC walimaliza wa nne na kupewa mipira mitatu.

Enock Babi wa Kigamboni FC alikuwa mfungaji bora wa bonanza hilo.

Twaha amesema Babi atawekewa kitita cha Sh 30,000 hadi 50,000 kwenye akaunti yake ya Meridianbet ambayo ataitumia kubashiri matokeo ili kujishindia mamilioni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles