30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Meno ya tembo yawapeleka jela

African_elephant_warning_raised_trunk

Na Walter Mguluchuma, Katavi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda imewahukumu watu wanne kifungo cha jumla ya miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na vipande 25 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 46 vikiwa na thamani ya Sh 371,600,000.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, baada ya  kuridhika na ushahidi uliotolewa na   upande wa mashtaka.

Washtakiwa waliohukumiwa kifungo  hicho ni mkazi wa Kijiji cha Ivungwe, Justine Baruti (39), wakazi wa Kijiji cha   Kalela kilichopo Kasulu mkoani Kigoma, Boniphace Hoza (40), Elias Hoza (46) na   mkazi wa Kijiji cha Ndurumo, Credo Gervas (45).

Upande wa mashtaka ukiongozwa na  Wakili wa Serikali Mkoa wa Katavi, Wakyo Simoni, ulikuwa na mashahidi 15 na washtakiwa walikuwa wakitetewa na  Wakili Elias Kifunda na washtakiwa  hawakuwa na mashahidi wowote zaidi yao.

Awali, Simoni alidai mahakamani hapo  kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Desemba 24, 2014 katika Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani iliyopo Mtaa wa Mji Mwema uliopo Manispaa ya Mpanda.

Simoni alidai kuwa siku ya tukio hilo, askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na Jeshi la Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa washtakiwa hao   wamepanga kusafirisha meno ya tembo  kutoka Mpanda na kuyapeleka Kigoma  kwa kutumia basi la Kampuni ya  Adventure Connection.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles