24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mengi aliliwa kila kona

Andrew Msechu –Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli ni miongoni mwa maelfu ya watu na taasisi mbalimbali waliomlilia Dk. Reginald Mengi kupitia mitandao ya kijamii huku wakieleza walivyomfahamu bilionea huyo.

RAIS MAGUFULI

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli aliandika: “Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha mzee na rafiki yangu Dk. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa letu na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha ‘I Can, I Will, I Must’. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara.”

NAPE NNAUYE

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye aliandika: “Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, rafiki, mshikaji, kiongozi na mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu cha mwisho nyumbani kwako}. Pumzika kwa amani Dr. R. A Mengi.”

BENKI YA DUNIA

Katika ukurasa wao, Benki ya Dunia Tanzania waliandika: “Benki ya Dunia inaungana na Watanzania katika kuomboleza kifo cha Reginald Mengi. Tunamheshimu kwa mchango wake katika maendeleo ya nchi. Pia tunaipa pole familia yake. Mungu amlaze pema, kwenye amani ya milele.”

JANUARY MAKAMBA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, naye aliandika: “Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins – na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi.”

UBALOZI WA ITALIA

Katika ukurasa wake wa Twitter, Ubalozi wa Italia nchini ulieleza: “Ubalozi wa Italia umepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha Reginald Mengi na unatoa salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na wafanyakazi wa IPP Media. Ubalozi utaendelea kumuenzi na kuendeleza uhusiano wa karibu na Mengi Foundation.”

UBALOZI WA MAREKANI

Katika taarifa yake kupitia Twitter, Ubalozi wa Marekani nchini uliandika: “Ubalozi wa Marekani umepokea kwa majozi makubwa taarifa za kifo cha Reginald Mengi asubuhi ya leo.

“Tulipata fursa ya kufanya kazi na Dk. Mengi katika siku zilizopita na kwa hakika mchango wake katika ukuaji wa muda mrefu wa uchumi na maendeleo ya Tanzania ni mkubwa na muhimu mno. Tunatoa pole na rambirambi zetu za dhati kwa familia na rafiki zake na kuungana na watu wa Tanzania katika kuomboleza msiba huu mzito.”

 

MWIGIZAJI LULU MICHEL

Naye mwigizaji Lulu Michel, kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika: “Binafsi nilianza kufahamika rasmi machoni pa watu katika tamthilia mbalimbali za Kaole Sanaa Group zilizokuwa zikirushwa na kituo cha ITV.  Pia ITV kama taasisi iligundua kipaji changu cha utangazaji na kunipa nafasi ya kuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto wetu kwa miaka kadhaa.
“R.I.P Chairman, ahsante kwa kuwa mmoja kati ya wengi walionipa nafasi ya kuonyesha kitu ambacho Mungu aliweka ndani yangu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles