MWANAMITINDO mwenye jina kubwa nchini Kenya, Annabel Onyango na meneja wa kundi la muziki la Sauti Sol, Marek Fuchs, wanataraji kufunga ndoa ya kihistoria nchini hapo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Kenyamoja, wachumba hao wa muda mrefu watafunga ndoa hiyo Septemba 19 na sherehe itafanyika katika hoteli ya Great Rift Valley tofauti na inavyofikiriwa kufanyika mjini ama kijijini kwao.
Wakati wote wa maandalizi ya harusi yao hiyo wapenzi hao wameweka kila kitu chao kitakachotokea kwa kila siku hadi siku ya ndoa yao kupitia mtandao wao.