Meneja Bandari ya Tanga aomba ushirikiano na wadau kuboresha ufanisi

0
1144
Meneja wa Bandari ya Tanga, Ajuaye Msese akizungumza katika kikao cha mwezi na wadau wa Bandari ya Tanga.

Mwandishi Wetu, Tanga

Wadau wa Bandari wametakiwa kushirikiana na Bandari ya Tanga ili kuifanya bandari hiyo kuwa bora zaidi na kimbilio katika kuwahudumia wateja wake kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika kikao na wadau hao, Meneja wa Bandari ya Tanga, Ajuaye Msese, amesema ushirikiano wa wadau hao ndiyo msingi wa maendeleo na kuiinua kibiashara bandari hiyo muhimu na yenye historia ya kipekee.

“Ushirikiano wenu wenye tija ndiyo utakaoleta ufanisi katika kuwahudumia ninyi na wateja wetu wengine kutoka ndani na nje ya nchi na bandari yetu iwe bora zaidi ya juzi, jana na leo,” amesema Msese.

Kikao hicho ni cha kwanza kwa meneja huyo kushiriki tangu ahamie Bandari ya Tanga akitokea Bandari ya Kigoma, kilijumuisha Wadau wote wanaohusika na upakiaji na upakuaji wa shehena katika Bandari ya Tanga ambapo
hufanyika kila mwezi.

Mmoja wa wadau wa Bandari ya Tanga akitoa maoni yake katika kikao hicho cha kila mwezi.

Vikao hivyo vinalenga kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa na Wadau wote walioko kwenye mnyororo wa kufanikisha upakiaji na upakuaji shehena bandarini uwe wenye tija na ufanisi ambapo lengo lake ni kukemea na kuondoa changamoto za kiutendaji na kimifumo zinazojitokeza wakati wa kuhudumia shehena zinazotoka na kwenda ndani na nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here