26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MELANIA TRUMP AFANYIWA UPASUAJI WA FIGO

MARYLAND, MAREKANI


MKE wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo kwenye Hospitali ya Taifa ya Kijeshi ya Walter Reed mjini Maryland.

Upasuji huo ulikuwa wenye mafanikio na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake juzi.

Melania (48), anatarajiwa kutumia muda mwingi wiki hii kupata nafuu hospitalini hapo.

Rais Trump aliandika katika Twitter kuwa alikuwa njiani kwenda kumtembelea hospitalini.

Wiki iliyopita, Melania alizindua mpango ujulikanao ‘Be Best’ wenye lengo la kuwafunza watoto kuhusu masuala ya kijamii, afya kuhusu hisia na kimwili.

Alisema kampeni hiyo ina lengo la kuhakikisha maisha yenye afya na kuzuia dhuluma.

Pia siku hiyo ilitangazwa kuwa aliyekuwa Kiongozi wa wengi wa Seneti wa Chama cha Democratic Harry Reid (78), alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kongosho.

Familia ya Reid ilisema madaktari kwenye hospitali ya Johns Hopkins Hospital huko Baltimore walikuwa na uhakika kuwa upasuaji huo ulikuwa wenye mafanikio na anapata nafuu vizuri.

Seneta wa Republican, John MacCain ambaye anaugua saratani ya ubongo ni kati ya wale waliomtumia ujumbe wa kumtakia heri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles