27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Meena: Sheria ya habari; ahadi ya Rais Samia imetimia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

“AHADI ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka wadau wa habari wakutane na kuchakata mapendekezo ya sheria za habari, imetimia. Hata kama bado kuna hatua zingine mbele, lakini hatua ya Wizara ya Habari kuitisha kikao na wanahabari na kisha kupitia mapendekezo, ni moja kati ya maagizo ya Rais Samia yametekelezwa,”.

Neville Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wakati akizungumza na Kituo cha Radio cha Dodoma (Dodoma FM) Agosti 18, 2022.

Ni kauli ya Neville Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wakati akizungumza na Kituo cha Radio cha Dodoma (Dodoma FM) Agosti 18, 2022.

Meena amesema kuwa: “Suala la mapendekezo yote ya wadau wa habari kupita, hilo ni suala lingine. Cha msingi ni kwamba, miongoni mwa ahadi za Rais (Samia), ikiwemo wizara kukutana na wadau wa habari na kupitia vifungu, imetekelezwa.

“Sisi kama wadau wa habari tunaamini tunakwenda kufanikiwa kwa kuwa, hata Waziri Nape (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) ana hisia chanya katika mchakato huo,’’ amesema Meena.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mapendekezo ya wadau wa habari katika mabadiliko ya sheria za habari nchini, ni kuwa uamuzi wa mahakama uwe unaheshimiwa.

Kwa ujibu wa Meena, baadhi ya vyombo vya habari licha ya kushinda kesi mahakamani lakini kumaliza vifungo vyao, Idara ya Habari Malelezo iligoma kuwapa leseni ili kuendelea na upashaji habai.

“Kuna gazeti (MwanaHalisi) licha ya kushinda kesi mahakamani, hawakupewa leseni ya kuendelea na uchapaji habari. Hao hao pia hata walipomaza kifungo bado hawakupewa leseni, jambo hili sio sawa hata kidogo,’’ amesema Meena.

Amesema, wadau wa habari nchini wamependekeza kwamba, mahakama inapotoa hukumu juu ya jambo fulani, basi serikali inapaswa kutekeleza kinyume na ilivyo sasa.

“Mkurugenzi wa Habari Maelezo anatumia sheria ile ile ambayo sasa inalalamikiwa ya kuwa na uamuzi wa kutoa leseni kwa chombo cha habari ama kutotoa kwa utashi wake.

“Katika hili tunapendekeza gazeti likishasajiliwa basi liendelee na kazi kwa kufuata taratibu zilizopo. Unapofunga chombo cha habari ksiendelee na kazi, unakuwa umeathiri wengi ikiwemo wafanyakazi na hata wasomaji,’’ amesema Meena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles