29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Meatu yapata milioni 800 ukamilishaji vyumba vya madarasa, zahanati

Na Derick Milton, Meatu

Halmashuari ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu imepokea kiasi cha zaidi ya Sh milioni 800 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa, vyoo, maabara, mabweni pamoja na zahanati.

Akitoa taarifa leo kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri Fabian Manoza, amesema kuwa fedha hizo tayari zimepokelewa na kupelekwa kwenye maeneo husika.

Manoza amesema kuwa serikali imetoa fedha hizo na kuziekeleza moja kwa moja kwenye maeneo yaliyokuwa na changamoto, ambapo katika sekta ya elimu kiasi kilichopokelewa ni zaidi ya Milioni 645 huku Afya zaidi ya Milioni 200.

Katika kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, Mkurugenzi huyo amewataka Madiwani hao kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata, kuhakikisha wanazisimamia kamati za ujenzi ambazo ndizo zitahusika katika kutumia fedha hizo.

“Fedha hizi zimeletwa kukamilisha baadhi ya sehemu ambapo wananchi walianzisha ujenzi lakini hawakukamilisha kama zahanati, lakini maeneo mengine ni kujenga madarasa mapya, kuna kukamilisha ujenzi wa maabara, vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na mabweni,” amesema Manoz.

“Madiwani pamoja na watendaji lazima muwe kitu kimoja kuhakikisha mnazisimamia kamati za ujenzi, kila hatua lazima zisimamiwe, na serikali imetoa maelekezo lazima thamani ya fedha ikaonekane na ubora wa mradi uwepo,” ameongeza Manoza.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo, Hadija Ally amesema kuwa katika mchanganuoa wa fedha hizo zitakamilisha jumla ya madarasa 11 shule za sekondari na madarasa 13 shule za Msingi.

Aidha Hadija ameeleza kuwa kuna ujenzi wa vyoo matundu 24, ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa katika shule za sekondari tatu, vyumba vinne shule za msingi, pamoja na ujenzi wa bweni moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles