27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MDEE, BULAYA KUKOSA BUNGE MWAKA MMOJA

Na KULWA MZEE-DODOMA


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya wote kutoka Chadema wamesimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya mkutano wa saba wa Bunge, nane na wa tisa, kwa kudharau mamlaka ya Spika.

Kutokana na uamuzi huo, wabunge hao hawatahudhuria vikao vya Bunge hadi mkutano wa 10 mwakani katika Bunge la Bajeti  la Aprili 2018/2019.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Bunge baada  ya kukubaliana na hoja ya kubadilisha maazimio ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyowasilishwa na  Mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza (CCM).

Kutokana na sakata hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kikosi cha askari kilichokuwapo bungeni Juni 2 mwaka huu na kushindwa kumtoa nje haraka Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), kimeondolewa na kuletwa kingine. Kikosi hicho kinadaiwa kilikuwa na askari zaidi ya 10.

Bulaya anatuhumiwa kudharau mamlaka ya Spika kwa kukaidi maelekezo yaliyomtaka kutulia kuruhusu mjadala wa

Wizara ya Nishati na Madini uendelee, ambapo alionekana akitangatanga na kuhamasisha wabunge wa upinzani kutoka nje.

Mdee alikuwa anatuhumiwa kudharau mamlaka ya spika kwa kufanya fujo kwa askari waliokuwa wameamuliwa kumtoa nje Mnyika kwa kuwavuta sare zao za kazi kwa lengo la kuwazuia kutekeleza amri halali ya Spika, kusimama na kuzungumza bungeni bila

kufuata taratibu za kanuni. 

Baada ya kuwasilisha mabadiliko hayo, Spikawa Bunge alihoji wabunge kama wanaafiki au hawaafiki,  lakini wabunge wengi waliafiki, hivyo mabadiliko hayo yalipita.

 

"Bunge limeafiki wabunge hao kutohudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa saba, nane na tisa wa Bunge.

 

“Katika hili moyo wangu mweupe kabisa, kwa muundo huu mwenye macho angependa kuona ataona, anayetaka kwenda kokote aende na maamuzi yoyote afanye, itakuwa chanzo cha mgogoro wa kikatiba.

"Mbunge wa Jimbo la Malindi, Ally Salehe (CUF) alisema yeye ndiye aliamrisha wabunge wengine watoke nje waende 

kujadiliana.

 

“Sina tatizo naye, katika kushauriana huko wengine waliropoka naomba nitoe onyo, wapo walionitukana mimi 

binafsi.

"Rhoda Kumchela (Viti Maalum Chadema) nakupa onyo kwa matusi, umekuja jana unanitukana, Mbunge wa Jimbo la Mlimba, 

Suzan Kiwanga (Chadema) na Katani Katani  Mbunge wa Jimbo la Tandahimba  (CUF)….mnanitukana nimewakosea  nini?,” ahoji Spika Ndugai.

Kwa upande wake Halima Mdee anatuhumiwa kudharau  mamlaka ya Spika kwa kuwafanyia fujo  askari waliokuwa wameamuriwa na spika kumtoa nje Mnyika.

"Umefika wakati sasa Bunge hili tukufu litoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wabunge hawa na wabunge wengine wote ambao wanafikiria hili ni genge ambalo mtu yeyote anaweza kulichezea na kulikosea heshima kila mara na kwa kadri anavyotaka.

 

KAMATI:

Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti wake,  Kapten George Mkuchika ilipeleka hati ya  kuwaita katika kamati wabunge hao kwa ajili ya kutoa ushahidi lakini hawakuwapa hati hiyo.

 

Alisema Polisi walipokwenda nyumbani walikuta taarifa kwa vijana wanaokaa nao kwamba wamesafiri na

waliagizwa wasipokee kitu chochote hivyo hati hizo ziliachwa na shauri liliamuliwa upande mmoja.

 

Baada ya kuchunguza tuhuma dhidi ya Bulaya na Mdee kamati ilitoa mapendekezo kwamba wabunge hao wasihudhurie vikao vyote

vilivyobaki vya mkutano wa saba na nane wa Bunge kutokana na tabia yao ya mara kwa mara ya kufanya vitendo vya kudharau mamlaka ya Spika.

 

Mkuchika alisema wabunge hao ni mara ya tatu kuitwa na kutiwa hatiani na kamati hiyo kwa  kosa la kudharau mamlaka ya Spika kwa makosa hayo ya awali na kwamba walishamaliza dhabu zote za kawaida wanazostahili kupewa kwa mujibu wa sheria

na kanuni za Bunge.

 

Wabunge hao walitenda makosa hayo Juni 2  wakati Bunge lilipokuwa likijadili hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara 

ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

 

Katika kikao cha Ijumaa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) wakati akichangia alisema inashangaza kuona wabunge wa upinzani wanatetea wezi wa rasilimali za taifa na kubeza jitihada za Serikali katika kukosemesha wizi huo.

Kutokana na maneno hayo Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alisimama na kuomba kutoa taarifa  kwa Lusinde kwamba si kweli kwamba wapinzani wanatetea wezi.

 

Lusinde aliporuhusiwa aendelee kuchangia, Mnyika alisimama tena na kuwasha kipaza sauti bila ruhusa na kudai  kuna mbunge aliyemuita mwizi, lakini Spika alimtaka akae chini bila mafanikio, ndipo Spika alipoamuru atolewe nje.

 

Michango

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), aliomba wasamehewe kwani hakukuwa na sababu ya shauri hilo kusikilizwa haraka. “Kamati itafute adhabu mbadala sio kila 

jambo mbunge afungiwe kuhudhuria vikao  kwani wanawakosesha wananchi fursa ya kuwakilishwa,” alisema.

 

Naye Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM),  aliunga mkono adhabu iliyopendekezwa na kamati kwamba inastahili hivyo aliwashauri wabunge wakubaliane nayo.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Hadija Aboud na Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM) walipendekeza adhabu iongezwe ikiwezekana warudi katika Bunge la Januari.

 

"Mdee mzoefu, haambiliki, inawezekana ni  malezi, spika inawezekana unalea  walioshindikana walipotoka, Bulaya tulikuwa  naye hakuwa hivi kabadilika," alisema Chatanda.

 

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) aliomba wabunge hao  wasamehewe kwani jambo hilo linahitaji 

busara kulishughulikia.

Katika hatua nyingine Ndugai aliwataka wabunge wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ili wananchi  wanaowaaongoza wakope na kuagiza apelekewe majina ya wabunge wote wanaodaiwa ili aweze kufuatilia na kuona hatua zinazoweza kuchukuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles